Timothy Ray Brown: Aliyekuwa mtu wa kwanza kutibiwa HIV amefariki


Timothy Ray Brown

Maelezo ya picha,

Timothy Ray Brown, pia alijulikan kwamba mgonjwa wa Berlin katika picha yake 2012

Mtu wa kwanza kutibiwa virusi vya ukimwi HIV – Timothy Ray Brown amefariki kutokana na saratani. Bwana Brown abaye pia alijulikana kama mgonjwa wa Berlin alipandikizwa uboho kutoka kwa mtu ambaye alikuwa ana kinga dhidi ya HIV 2017.

Hii ilimaanisha kwamba alikuwa ahitaji tena dawa za kukabiliana na virusi vya ukimwi hivyobasi alisalia bila maambukizi yoyote ya virusi hivyo vinavyosababisha ukimwi kwa maisha yake yote.

Shirika la kimataifa kuhusu msaada duniani limesema kwamba bwana Brown aliupatia ulimwengu matumaini kwamba dawa ya kutibu ukimwi inaweza kupatikana.

Bwana Brown mwenye umri wa miaka 54, ambaye alizaliwa nchini Marekani , alipatikana na virusi vya HIV alipokuwa akiishi Berlin 1995.

Na baadaye mwaka 2007 alipata saratani ya damu kwa jina Myeloid Leukemia. Tiba yake ilianza kuharibu uboho wake ambao ulikuwa ukizalisha seli hizo za saratani kabla ya kufanyia upandikizaji wa uboho.

Uboho huo ulitoka kwa mfadhili ambaye alikuwa na mabadiliko nadra katika sehemu ya DNA iitwayo jeni ya CCR5.

Kinga dhidi ya HIV

CCR5 ni seti yenye maagizo ya jeni ambayo huunda mlango ambao virusi vya ukimwi (VVU) huingia kuambukiza seli.

Mabadiliko ya CCR5 kimsingi hufunga mlango na kuwapa watu kinga dhidi ya VVU.

Niliwacha kula dawa siku ambayo nilifanyiwa upandikizaji , na baada ya miezi mitatu sikuwa na virusi vya ukimwi mwilini mwangu. Bwana Brown aliambia BBC mwaka 2012.

” Virusi havikugundulika mwilini mwake tena. Kwa kweli alikuwa “amepona”.

Lakini saratani ya damu ambayo ilisababisha kupona VVU, ilirudi mapema mwaka huu na kuenea kwenye ubongo wake na uti wa mgongo.

“Ni kwa masikitiko makubwa kwamba ninatangaza kifo cha Timothy ambaye aliaga dunia … akiwa amezungukwa na mimi na marafiki, baada ya vita vya miezi mitano na saratani ya damu,” mwenzake Tim Hoeffgen aliandika kwenye Facebook.

Aliongeza: “Tim alitumikia maisha yake kusimulia hadithi yake juu ya tiba yake ya VVU na kuwa balozi wa matumaini.”

Je tunakaribia kupata tiba?

Tiba ya Bwana Brown ilikuwa hatari sana kutumika mara kwa mara – inasalia kuwa tiba ya saratani.

Njia hiyo pia ni ghali sana kwa watu milioni 38, wengi wanaoishi katika jangwa la sahara wanaofikiriwa kuishi na maambukizi ya VVU.

Walakini, hadithi ya Bwana Brown iliwapatia msukumo wanasayansi, wagonjwa na ulimwengu kwamba tiba inaweza kupatikana.

Jumuiya ya Ukimwi ya Kimataifa (IAS) ilisema ilikuwa ikiomboleza na “moyo mzito sana”.

” Timothy na daktari wake, Gero Hutter, wanatudai shukrani kubwa kwa kufungua mlango kwa wanasayansi kuchunguza dhana kwamba tiba ya VVU inaweza kupatikana,” alisema Prof Adeeba Kamarulzaman, rais wa IAS.

Mgonjwa wa pili aliyepona VVU alitangazwa mapema mwaka huu. Adam Castillejo – anayejulikana kama mgonjwa wa London – alipatiwa matibabu sawa na yale ya Bwana Brown na aliwacha kutumia dawa zake za VVU.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *