Trump na Kim wakubaliana kuanza tena mazungumzo


Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un

Haki miliki ya picha
Getty Images

Donald Trump amekuwa Rais wa kwanza wa Marekani kuingia nchini Korea Kaskazini, baada ya kukutana na Kim Jong-un kwenye eneo linalotenganisha Korea Kaskazini na Kusini.

Nchi hizo mbili zimekubaliana kufufua mazungumzo kuhusu nyukilia yaliyokuwa yamesimama.

Mkutano wao wa mwisho ulivunjika mwezi Februari huku kukiwa hakuna maendeleo yeyote kuhusu mpango wa kusitisha utengenezaji wa silaha za nyukilia.

Wakosoaji wanaona kuwa kukutana kwa viongozi hao kwa mara ya tatu kwa kipindi cha mwaka mmoja kama mchezo wa kisiasa na kusema kuwa Korea Kaskazini bado wanapaswa kuonyesha kuwa wamedhamiria kuachana na silaha za nyukilia.

Katika mkutano ambao hatimaye ulipangwa kufanywa baada ya Trump kumualika Kim kwenye ukurasa wake wa Twitter siku ya Jumamosi, walisalimiana kwa kushikana mikono katika eneo la mpaka kati ya Korea zote mbili kabla ya bwana Trump kuvuka kuingia Korea Kaskazini.

Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

Rais wa Marekani Donald Trump na wa Korea Kusini Moon Jae-in walikutana kuzungumza

”Ni vyema kukuona tena.Sikutarajia kukutana nawe hapa,” Bwana Kim alimwambia Trump huku akitabasamu.Tukio la kukutana kwao lilionyeshwa moja kwa moja na televisheni ya kimataifa.

”Ni wakati muhimu,” alisema Trump, ”maendeleo makubwa.”

Kukutana kwao mwanzoni ilielezwa kuwa ni kwa muda mfupi, lakini Trump na Kim waliongea kwa takriban saa moja, upande wa Korea Kusini.

Kwa muda mfupi, Trump na Kim waliungana na Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in.

Kim aishutumu Marekani kwa ‘kupotosha ukweli’

Marekani yaikamata meli ya Korea Kaskazini

Akizungumza na wanahabari akiwa pembeni ya Trump, Kim amesema mkutano wao ni ishara ya uhusiano wao ”mzuri sana”.

Akiita urafiki wao ”mzuri”, Trump ambaye awali alimuita Kim ”mtu wa roketi”- amesema ni ”siku nzuri kwa dunia” na kwamba ”anajivunia kufika kwenye mpaka” wa nchi hizi za Korea.

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Trump na Kim wakipeana mikono wakiwa kwenye mpaka wa Korea Kaskazini

Marais mbalimbali wa Marekani walitembelea eneo la mpaka linalogawanya peninsula tangu kumalizika kwa vita ya Korea mwaka 1953, kuonyesha kuiunga mkono Korea Kusini.

Rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter na Bill Clinton walishawahi kutembelea Korea Kaskazini, mjini Pyongyang-lakini baada ya kuondoka madarakani.

Trump alionekana kufurahia sana tukio hili la kufika kwenye eneo la mamlaka ya nchi ambayo kwa muda mrefu, imekuwa adui.

Mahusiano haya yamepunguza mzozo kwenye peninsula ya Korea, lakini hayajafanya Korea Kaskazini kusitisha mradi wake wa kutengeneza silaha za nyukilia.

Haki miliki ya picha
Reuters

Uhusiano wao umefanya kuwepo kwa matabasamu na kushikana mikono, lakini si kusitishwa kwa utengenezaji wa siaha za nyukilia katika eneo la peninsula ya Korea.

Ushawishi unaendelea?

Wapatanishi kutoka pande zote mbili watakutana wiki zijazo kuanza mazungumzo kuhusu mradi wa nyukilia wa Korea Kaskazini, Trump amewaambia waandishi wa habari, akisema ”hatafuti kasi ya kufikia malengo, bali kutekeleza vyema malengo.”

Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini, aliongeza, vitaendelea kuwepo ingawa kuna uwezekano wa kupunguza ikiwa sehemu ya mazungumzo.Trump amesema amemkaribisha Kim kutembelea Washington.

Wachambuzi wa mambo wana mashaka kama mkutano huu utazaa matunda hasa kuhusu kukomesha uzalishaji wa silaha za nyukilia.

Haki miliki ya picha
AFP

Uhusiano wa Marekani na Korea Kaskazini ukoje?

Mazungumzo na Korea Kaskazini kujaribu kuishawishi kuachana na mradi wa nyukilia ambao ulifikia kilele mwaka jana wakati Trump na Kim walipokutana nchini Singapore.

Kwa pamoja waliahidi kuachana na mpango wa kutengeneza silaha za nyukilia, lakini bila kufafanua walimaanisha nini?

Kulikuwa na matumaini kuwa mkutanno wa Hanoi mwezi Februari ungewafanya viongozi hao wafikie makubaliano ya Korea Kaskazini kuachana na mradi wa nyukilia ili kuondolewa vikwazo.

Lakini mazungumzo hayo hayakuwafanya kufikia makubaliano yoyote, kwa kuwa walishindwa kukubaliana kwa amani kuhusu vikwazo vipi vingepatiwa unafuu. Tangu kukwama kwa mazungumzo, rais Trump na Kim hivi karibuni wamekuwa wakiwasiliana kwa barua.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *