Tundu Lissu kupinga uamuzi wa kuufuta ubunge wake


''Sasa ninaweza kuwafahamisha kwamba mimi na timu ya mawakili wangu tuko tayari kuingia Mahakama Kuu ya Tanzania'' amesema Lissu

Image caption

”Sasa ninaweza kuwafahamisha kwamba mimi na timu ya mawakili wangu tuko tayari kuingia Mahakama Kuu ya Tanzania” amesema Lissu

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu amesema kuwa yuko tayari kupinga mahakamani uamuzi wa kumuondolea sifa ya ubunge kinyume cha sheria.

Lisu ambaye aliwahi kuwa Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni nchini humo , Tundu Lissu amesema Jumanne hatumii tena dawa wala magongo kutembea na baada ya Agosti 20, 2019 atakuwa tayari kurejea nchini mwake kutoka Ubelgiji aliko sasa.

Mwanasheria huyo Mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Tundu Lissu amesema amehitimisha matumizi ya dawa alizoanza kuzitumia tangu Septemba 7 mwaka 2017.

Lissu alianza kutumia dawa hizo Septemba 7 mwaka 2017 baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa katika makazi yake Area D jijini Dodoma ambapo tangu wakati huo amekuwa akipatiwa matibabu nje ya nchi.

Haki miliki ya picha
Bunge

Image caption

Spika wa Bunge la tanzania Job Ndungai

Juni 28, 2019 Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alilieleza Bunge kuwa Lissu amepoteza sifa hizo kwa sababu mbili, mkiwemo kutokujaza fomu za mali na madeni kwa viongozi wa umma na kutokutoa taarifa kwake ya wapi alipo.

Akizungumzia suala hilo, Lissu amesema tangu alipopoteza ubunge, “sijasema maneno mengi sana, zaidi ya kusema kwamba tutaenda Mahakama Kuu kupinga uamuzi huo.”

“Kesi za ubunge, kama zilivyo kesi zote za uchaguzi wa kisiasa, ni kesi za kisiasa. Ni mwendelezo wa mapambano ya kisiasa katika uwanja tofauti. Kwa sababu hiyo, ni kesi nyeti na za kipekee sana. Zinahitaji umakini mkubwa katika kuziandaa na kuziendesha. Nina uzoefu mkubwa nazo, kwa sababu nimezifanya sana tangu 2005.”

“Sasa ninaweza kuwafahamisha kwamba mimi na timu ya mawakili wangu tuko tayari kuingia Mahakama Kuu ya Tanzania. Tutafanya hivyo muda wowote kuanzia leo. Maandalizi yote yanayohitajika yamekamilika,” amesema Lissu.

Amesema tunataka kuiomba Mahakama Kuu itoe jibu la swali alilouliza Spika Ndugai na walio nyuma yake: je, Spika wa Bunge la Tanzania ana uwezo kikatiba na kisheria wa kufuta ubunge wa mbunge yeyote yule, kwa sababu yoyote ile, bila kumuuliza mbunge husika jambo lolote kuhusu sababu za kumfuta ubunge huo???

“Nitawajulisheni mara moja kesi hii itakaposajiliwa rasmi. Kama itawapendeza, nitawaomba mtakaopata nafasi kuhudhuria mahakamani, kwa niaba yangu, wakati wote kesi hiyo itakapokuwa inaendelea,” amesema

Image caption

Lissu amesema kwa maelekezo ya madaktari wake Jumanne wiki hii ilikuwa siku ya mwisho ya mimi kutumia dawa ambazo alizitumia tangu siku aliposhambuliwa

Katika salamu kwa marafiki zake alizozitoa Jumatano , Lissu ameanza kwa kuzungumzia afya yake akisema, “Leo Julai 31, 2019 ni siku ya kwanza tangu niliposhambuliwa Septemba 7, 2017, situmii dawa ya aina yoyote.”

“Kwa maelekezo ya madaktari wangu, jana (Jumanne) ilikuwa siku ya mwisho ya mimi kutumia dawa ambazo nimezitumia tangu siku niliposhambuliwa,” amesema mbunge huyo wa zamani wa Singida Mashariki.

“Na jana hiyohiyo nilitimiza mwezi mzima tangu niache kutumia magongo. Ijapokuwa bado nachechemea kwa sababu ya goti kutokukunja sawasawa, sasa ninatembea bila msaada wa magongo,” amesema

Katika salamu zake, Lissu amesema, “Safari yangu na yetu, ndefu ya matibabu itakamilika Agosti 20,2019 nitakapokutana na timu ya madaktari wangu kwa ajili ya vipimo vya mwisho na ushauri. Baada ya hapo itakuwa ni maandalizi ya kurudi kwetu. Hakutakuwa na sababu tena ya kitabibu ya mimi kuendelea kukaa Ulaya.”

Amesema kwa vile tumekuwa pamoja kwenye safari hii ndefu, hatuna budi kupongezana na kumshukuru Mungu kwa hatua hii nzuri nilikofikia.

“Mimi na familia yangu hatutachoka kuwashukuru sana kwa kuwa pamoja nasi katika kipindi chote hiki kigumu. Mungu awabariki sana.” amesema Lisu.

Image caption

Kiongozi wa Chadema Freeman Mbowe alithibitisha kuwa Tundu Lissu alisema atarudi nchini Tanzania tarehe 07.09.2019 kuadhimisha siku ya kushambuliwa kwake

Mnamo mwezi Mei mwaka huu katika mahojiano na Televisheni ya Chadema mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe katika makao makuu ya Chadema Lisu alisema kuwa atarudi nchini Tanzania tarehe saba mwezi wa tisa ili kuadhimisha kushambuliwa kwake.

”Nitatua tarehe saba mwezi septemba 2019 kwenye ardhi ya tanzania kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nitakuwepo, alisema Tundu Lissu

Tangazo hilo liliwafurahisha sana wanachama wa chama hicho waliokuwa katika makao makuu ya chama hicho.

Mbowe alisema kuwa utaratibu wa mapokezi yake utapangwa na kutangazwa kitaifa.

Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma, katikati mwa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa ya chama kikuu cha upinzani CHADEMA kwa vyombo vya habari, tukio hilo lilitokea wakati mbunge huyo wa Singida Mashariki alipokuwa nyumbani kwake.

Tundu Lisu ni miongoni mwa wanasiasa wa upinzani nchini Tanzania ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Tanzania.

Ametangaza kwamba yuko tayari kuwania urais 2020 iwapo vyama vya upinzani vitamridhia kufanya hivyo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *