“Twende Kileni”: Msanii Diamond Platinumz arudia njiani?


Wasanii wa Tanzania

Haki miliki ya picha
The Citizen

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul maarufu Diamond Platinumz ni mmoja wa wasanii walioshiriki kampeini ya kupanda mlima Kilimanjaro mwaka huu lakini hakufanikiwa kufika kileleni.

Licha ya hatua ya msanii huyo kuangaziwa pakubwa katika mitandao ya kijamii alirudi baada ya kufika kituo cha kwanza.

Kampeini hiyo ambayo imekua ikihamasisha baadhi ya raia kutoka nchini Tanzania, wasanii, viongozi mbali mbali na hata raia wa kawaida kujitokeza kuenda kupanda mlima kilimanjaro imekua ikiendelea kwa wiki moja sasa.

Kampeini hiyo ilikua ikiendeshwa chini ya Waziri wa Malia asili na Utalii Daktari Hamisi Kigwangala ikiwa na kauli mbiou ya Tukutane Kileleni.

Baadhi ya wasanii kutoka nchini Tanzania akiwemo balozi wa Utalii Miss Tanzania Queen Elizerbeth walifanikiwa kupanda mlima huo kwa wakati wake wakiandamana na waziri Kigwangala.

Wasanii wa filamu za Bongo movie Steve Nyerere na Steve Jacobs pia waliojitoa kituo cha kwanza kuelekea mpango wa kukwea mlima Kilimanjaro.

Kili Challenge ni mfuko ambao umeendelea kukusanya fedha nyingi kwa miaka yote, fedha ambazo zimetumika kusaidia maeneo mbalimbali na makundi ya Wajane, Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI, Watoto yatima, Vijana, pamoja na Taasisi zinazotoa huduma muhimu za UKIMWI nchini.

Tatizo la UKIMWI kwa Tanzania bado ni kubwa kwani kutokana na takwimu zilizopo kuonyesha kwa kila mwaka takriban watu 72,000 hupata maambukizi mapya ya VVU. Takriban watu milioni 1.5 wameambukizwa na VVU kwa hiyo wastani wa hali ya maambukizi ni sawa na asilimia 4.7 kwa Tanzania bara.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *