Uganda: 'Ilibidi nivue nguo kuthibitisha jinsia yangu'


Cleopatra Kamburu
Maelezo ya picha,

Cleopatra Kamburu anasema ilikuwa aibu kubwa kutakiwa kuvua nguo ili athibitishe jinsia yake.

Cleopatra Kamburu anasema ilikuwa aibu kutakiwa kuvua nguo zake ili kuonyesha yeye ni nani. Uganda imetoa kitambulisho cha kwanza kwa watu waliokumbatuia jinsia tofauti na waliozaliwa nayo(Transgender)

Kwa neno la kiingereza ‘transgender’ ni mtu mwenye hisia tofauti na maumbile yake ya asili, kama mwanaume anakuwa na hisia za kike kama mwanamke anakuwa na hisia za kiume na wengine wengi kubadili jinsia zao kabisa.

Wiki iliyopita Cleopatra Kamburu alikabidhiwa hati yake mpya ya kusafiria na kitambulisho chake, kikimtambulisha kama mwanamke.

Ameiambia BBC kwamba alikuwa na matumaini kitambo kwamba siku moja ingewezekana kutambuliwa. Lakini kupata hati na nyaraka hizo kulionekana kama hatua muhimu katika historia, sawa na wakati wanawake waliporuhusiwa kupiga kura kwa mara ya kwanza.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *