Ujerumani haitasusia Kombe la Dunia la 2022 huko Qatar


Akitaja “maelewano ” yanayopatikana. Peter amesema hana sababu “ya kutilia shaka” juu ya mwenendo wa Qatar.

Ujerumani ilikuwa timu ya kwanza ya taifa kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2022 huko Qatar baada ya kuifunga Macedonia Kaskazini 4-0 huko Skopje siku ya Jumatatu. Soma Blatter aitaka Qatar kuheshimu haki za wafanyakazi

Mapema Jumatatu, shirikisho la soka la Ujerumani (DFB) lilichapisha mahojiano kwenye tovuti yake, ambapo makamu wa rais Peter Peters aliulizwa juu ya uwezekano wa Ujerumani kususia mashindano hayo kwa sababu ya rekodi ya ukiukaji wa haki za binadamu ya Qatar.

“Licha ya kutakiwa na wengine kususia, hakutaleta [Qatar] na watu wake mbele, Mashirika yasiyo ya kiserikali na wataalam wengine wamethibitisha katika majadiliano yetu kwamba Qatar ni ardhi ya mpito.” alisema Peter Peters mkurugenzi wa zamani wa Schalke.

Peters ameongeza kuwa Qatar imeshuhudia “maendeleo mengi mazuri” katika miaka michache iliyopita, na ni jukumu la mashabiki wa mpira wa miguu kusaidia maendeleo hayo.

Siku moja kabla ya mahojiano hayo kuchapishwa, ripoti nchini Ujerumani iliashiria taswira tofauti ya mtazamo huko Qatar. Kulingana na kipindi cha michezo cha upelelezi cha Spoti Inside, kinachopepereshushwa na kituo cha umma WDR, wafanyikazi wa kigeni nchini Qatar bado wanakabiliwa na masuala mengi ambayo mamlaka inadai kuwa inashughulikia. soma Tarehe za Kombe la Dunia Qatar 2022 zachaguliwa

Kulingana na ripoti hiyo, kampuni nyingi bado hazilipi mshahara wa chini wa riyali 1,000 za Qatar ($ 275, € 240) kwa mwezi, na wafanyikazi wengi bado wanacheleweshewa mishahara yao.

Kususia michuano ya Qatar

DFB Vize-Präsident Peter Peters

Mkurugenzi wa DFB-Peter Peters

Nchini Ujerumani, wito wa kususia Kombe la Dunia la 2022 huko Qatar umepata uungwaji mkono kutoka kwa waliomo katika ulingo wa soka na jamii.

Kura ya maoni iliyofanywa mnamo Machi 2021 na jarida la Der Spiegel iligundua kuwa 54% ya Wajerumani wanaunga mkono kususia, na 14% zaidi wakiunga mkono kwa masharti. Kwa kuongezea, 72% walisema wangetaka DFB iwe na sauti zaidi katika kukosoa hali ya haki za binadamu huko Qatar.

Kura nyingine ya maoni ya shirika la utangazaji la umma WDR, iligundua kuwa 65% ya Wajerumani wanaamini Ujerumani haipaswi kushiriki Kombe la Dunia la 2022. soma Neymar kutundika daluga baada ya Kombe la dunia?

Mashabiki pia walikuwa na maoni yao juu ya ushiriki wa Ujerumani kwenye mashindano hayo. Shirika la ProFans, lilidai kwamba DFB isishiriki Kombe la Dunia la 2022 kutokana na hali ya haki za binadamu nchini humo, na kuyataja mashindano hayo kama “tamasha la kifahari la mpira wa miguu kwenye makaburi ya maelfu ya wahamiaji.”

Maandamano nje ya uwanja

Deutschland München | UEFA Euro 2020 | Frankreich v Deutschland

Mashabiki wa timu ya taifa ya Ujerumani

Kulingana na shirika la ProFans, Kwa Ujerumani katika Kombe la Dunia la Qatar kungeashiria “mwisho wa maadili na utu.”

Mashabiki waliojipanga kote Ujerumani wamekuwa wakipinga kuhusika kwa nchi hiyo katika mpira wa miguu wa Ujerumani, haswa ikihusiana na makubaliano ya udhamini wa Bayern Munich na shirika la ndege la Qatar Airways.

Kulingana na gazeti la kila siku la Uingereza la The Guardian, jumla ya wafanyikazi wageni 6,500 wamekufa nchini Qatar tangu taifa hilo lilipotangazwa kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia mnamo 2010.

 

 

Chanzo: https://p.dw.com/p/41Zwd Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *