UN yawaondoa wakimbizi 149 wa Kiafrika waliokuwa hatarini LibyaUNHCR iliwafikisha wale wote waliondolewa Libya katika eneo karibu na Rome, taarifa imeeleza. Watu hao ambao ni wahamiaji kutoka Eritrea, Somalia, Sudan na Ethiopia – wakiwemo watoto 65. Kumi na tatu ni watoto wneye umri chini ya mwaka mmoja.

Watu hao waliosafirishwa kutoka Libya walikuwa wako kizuizini katika mazingira mabaya mjini Tripoli, UNHCR imesema. Wakati hali ya usalama ikiendelea kuwa mbaya, UN imeshirikiana na vyombo vya usalama vya Libya na Italia kuwaondosha watu hao.

Balozi wa Somalia nchini Libya, Muhiyadin Mohamed Kalmoy amesema kuwa wakati Tripoli ikiwa haina utulivu, UNHCR ilikuwa inauwezo zaidi kuliko wanadiplomasia wa nchi za kigeni kuwatafutia mahali pa kwenda wakimbizi wa Kiafrika na kuwapeleka maeneo salama.

“Raia wa Somalia ambao ni miongoni mwa watu walioondolewa walikuwa wamewasiliana nasi kupitia taasisi nyingine kutufahamisha hali inayowakabili,” Kalmoy ameiambia VOA Ijumaa, “ lakini tulikuwa hatuna njia ya mawasiliano rasmi kutoka UNHCR juu ya wale waliopelekwa Rome.”

Kalmoy amesema serikali yake ilikuwa inashughulikia kuhakikisha usalama na kuthibitisha uraia wa wananchi wetu” na kuisaidia UNHCR na Mashirika ya Kimataifa yanayo simamia Wakimbizi (IOM) kushughulikia kesi za wale ambao wanaweza kurudi “Somalia au kupata hifadhi nchi nyingine.”

Hata hivyo alikuwa hajui, mpaka siku ya Ijumaa, idadi kamili ya raia wa Somali waliopelekwa Rome.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *