Urusi yajiandaa kwa maandamano makubwa ya mpinzani uawala wa Urusi Alexei Navalny


A view of a large poster depicting Russian opposition leader Alexei Navalny

Maelezo ya picha,

Zaidi ya watu 4,000 walikamatwa katika mkutano mkubwa wa kumuunga mkono Alexei Navalny wiki iliyopita

Mamlaka nchini Urusi zimefunga vituo vya treni na basi vya abiria na kuzuwia shughuli za watu katika mji mkuu wa nchi hiyo Moscow kabla ya mkutano maandamano makubwa yakiyopangwa kwa ajili ya kumuunga mkono kiongozi wa upinzani na mkosoaji wa utawala Urusi Alexei Navalny.

Migahawa mingi na maduka katikati ya mji huo vitafungwa na usafiri wa treni wa chini ya ardhi utabadilishwa.

Zaidi ya watu 4,000 walikamatwa kote nchini Urusi wakati wa mikutano wiki iliyopita.

Bw Navalny alifungwa jela aliporejea nchini Urusi baada ya kupona jaribio la kumuua kwa sumu inayoua neva.

Mpinzani huyo wa serikali ya Urusi alitakamtwa tarehe 17 Januari kwa kutotimiza masharti ya hukumu iliyoahirishwa dhidi yake . Alikuwa ndio amewasili tu kutoka mjini Berlin, ambako aliishi kwa miezi kadhaa akiendelea kupona shambulio la sumu ambalo nusura limuue.

Unaweza pia kusoma:

Mamlaka nchini Urusi zinasema kuwa alipaswa kuripoti polisi kwasababu ya kesi yake ya ubadhilifu wa mali ya umma iliyoahirishwa.

Bw Navalny alipinga kukamatwa kwake jambo ambalo anasema “ni ukiukaji wa sheria “, na kuongeza kuwa mamlaka zinafahamu fika kwamba alikuwa akitibiwa mjini Berlin kutokana na sumu ya Novichok , ambayo alipewa Urusi mwezi Agosti mwaka jana.

Maelezo ya picha,

Muandamanaji katika mji wa Vladivostok akiwa amevalia barakoa iliyoandikwa : “Putin lazima ajiuzulu”

Nini kinachoendelea kwa sasa?

Maandamano makubwa ya kumuunga mkono Bw Navalny yameanza kufanyika nchini Urusi , licha ya onyo jipya kutolewa na polisi kuhusu mikusanyiko ya watu ambapo polisi wanawashikilia watu zaidi ya 250 , kwa mujibu wa kikundi cha maandalizi ya maandamano hayo OVD-Info protest monitoring group. Maandamano katika mji mkuu Moscow yanatarajiwa kufanyika baadae leo.

Washirika kadhaa wa Bw Navalny wamekuwa wakifungwa tangu juma lililopita na wengine , akiwemo kaka yake na mwanaharakati wa kikundi cha Pussy Riot Maria Alyokhina, ameweka katika kifungo ha ndani.

Mhariri mkuu wa wavuti wa Urusi uliobobea katika masuala ya haki za binadamu , Sergei Smirnov, alikamatwa nje ya nyumba yake Jumamosi. Taarifa za kukamatwa kwake kutokana na tuhuma za kushiriki katika maandamano ya wiki iliyopita , zimelaaniwa vikali na waandishi wa habari wengine nchini humo.

Mjini Moscow, wameripotiwa kuhangaika kupata nafasi katika jela kwa ajili ya wafuasi wa kiongozi huyo wa upinzani.

Vituo saba vya safari za leri vitafungwa leo Jumapili na matembezi ya raia yatadhibitiwa katikati mwa mji wa Moscow , limeripoti shirika la habari la AFP.

Maelezo ya picha,

Polisi wmeripotia kuhangaika kupata chumba katika gereza kwa ajili ya wafuasi wa Ravanly

Mandamano yanatarajiwa katka maeneo mengine ya nchi [ia, licha ya kwamba viwango vya joto vimeshuka hadi – nyuzijoto -52 .

Katika mji wa Vladivostok, mashariki mwa Urusi, washirika wa Bw Navalny wanasema hakuna maandamano ya kiwango cha Jumamosi yaliyowahi kutokea kwa kipindi cha muongo mmoja.

Bw Navalny anawalaumu maafisa wa usalama wa taifa kwa kutekeleza maagizo ya Bw Putin kwa kumshambulia n kwa sumu ya Novichok ambayo ilikaribia kumuua. Waandishi wa habari wa taarifa za uchunguzi kutoka Bellingcat waliwataja maafisa wa Shirika la upelelezi la Urusi wanaoshukiwa kumpa sumu Bw Navanly

Utawala wa Kremlin unakanusha kuhusika shambulio hilo la sunu na unapinga matokeo ya uchunguzi ya wataalamu wa silaha kutoka nchi za Magharibi, waliosema kwamba sumu ya Novichok ilitumika dhidi ya Navanly.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *