Uswisi kuruhusu kwa mara ya kwanza wanajeshi wanawake kuvaa nguo za ndani za kike


Uswisi ina matumaini ya kuwatia moyo wanawake kujiunga na vikosi vya kijeshi

Chanzo cha picha, IMAGE COPYRIGHTFABRICE COFFRINI/GETTY IMAGES

Uswisi itawaruhusu wanajeshi wanawake kuvaa nguo za ndani za kike kwa mara ya kwanza katika jitihada za kuongeza idadi kubwa ya wanawake wanaojiunga na jeshi, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Chini ya mfumo wa sasa, sare za jeshi zinazotakiwa kwa wanawake wanaojiunga na jeshi zinahusisha, nguo za ndani za kiume.

Majaribio , yatakayoanza mwezi ujao, yatahusisha sare za jeshi zenye nguo za ndani za wanawake za majira ya joto na za miezi ya baridi.

Wanawake ni sehemu ya takribani 1% ya jeshi la Uswisi, lakini nchi hiyo ina matumaini ya ongezeko la mpaka 10% ya wanawake ifikapo mwaka 2030.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *