Utafiti:Mbwa wanaweza kubaini dalili za kifafa kwa kunusa kwa kutumia pua yake


Pua ya Mbwa

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Utafiti huu ni msaada mkubwa kwa wagonjwa wa kifafa, katika kubaini mapema kabla ya athari kujitokeza

Wanasayansi wa Ufaransa wanasema wana ushahidi kuwa Mbwa anaweza kuhisi dalili za ugonjwa wa kifafa.

Timu ya Chuo Kikuu cha Rennes kina matumaini kuwa uvumbuzi wao utawezesha wataalamu kubaini mtu mwenye dalili za ugonjwa wa kifafa.

Inaweza kuwa mbwa au pua za ”kielektroniki ” zinazoweza kunusa harufu inayotoka kwa mtu mwenye dalili ya ugonjwa wa kifafa.

Mbwa awali walionyesha kuwa na uwezo wa kunusa harufu zinazoashiria kuwepo kwa dalili ya maradhi kadhaa ikiwemo saratani, Malaria na sukari.

Baadhi ya watu wenye kifafa huwategemea wanyama.

Mnyama mmoja akiwa kwenye chumba alicholala mtoto, anaweza kuitahadharisha familia kuwepo kwa dalili ya kifafa wakati wa usiku wa manane.

Katika utafiti wa hivi karibuni, ulioandikwa katika jarida la ripoti za kisayansi, mbwa watano walipata mafunzo nchini Marekani kubaini harufu ya jasho la mtu aliye na kifafa.

Jinsi pombe inavyoathiri jeni zako na kukupa hamu ya kubugia zaidi

Je wajua kwamba usingizi huathiri maisha yako?

Hatua ya kwanza

Mbwa wawili kati yao walibaini dalili za kifafa karibu kiasi che theluthi mbili na wenine watatu walikua wamepatia kwa asilimia 100.

Ripoti inasema:”majibu yako wazi kabisa na ilihusisha kubaini harufu ya mtu mwenye dalili ya kifafa.

lakini haijulikani ni kwa vipi dalili za kifafa zinaonekana katika mabadiliko ya harufu.

Daktari Amelie Catala, wa Chuo Kikuu cha Rennes ameiambia BBC: ”Utafiti zaidi unahitajika lakini inawezekana kuwa mabadiliko mwilini husababisha kutoka kwa homoni zinazosababisha kutoa harufu ya aina ya tofauti, lakini nadharia hii bado iko kwenye majaribio.

Hata hivyo utafiti huu unaelezwa kuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa.

Ripoti inasema itasaidia kuboresha namna ya kutambua dalili za kifafa mapema zaidi.

hali itakayoweza kumsaidia mtu kuomba msaada au kujiondoa kwenye maeneo ya hatari kabla ya kuanguka kifafa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *