Viongozi wa EAC kukutana leo, Arusha


Marais wa Kenya, Uganda na Tanzania

Haki miliki ya picha
IKULU TANZANIA

Image caption

Marais wa Kenya, Uganda na Tanzania

Viongozi wa Jumuia ya Afrika ya Mashariki wanakutana baadaye leo mjini Arusha kaskazini mwa Tanzania, huku kukiwa na hali ya wasiwasi na uadui miongoni mwa nchi wanachama.

Katika siku za hivi karibuni Burundi iliitangaza Rwanda kama adui yake. Na kwa upande mwingine Rwanda imekuwa ikilalamikia juu ya kile inachosema vitendo vya utesaji, utekwaji na kurudishwa nyumbani kiholela kwa raia wake wanaosafiri nchini Uganda.

Wanachama wengine wa jumuia hiyo ya EAC ni pamoja na wenyeji wa mkutano Tanzania, Kenya na Sudan ya Kusini.

Sio viongozi wote wa mataifa sita wanachama watahudhuria mkutano huo wa leo. Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza atawakilishwa na naibu wake, wakati Rais wa Sudan kusini Salva Kiir naye atawakilishwa na ujumbe maalum.

Mkutano huu ulipangwa kufanyika Novemba mwaka jana lakini ukaahirishwa mara mbiili baada yab Burundi kuugomea. Burundi inalalamika kwamba jumuia inafumbia macho uhusiano wake mbaya na Rwanda, ambayo kwa sasa ndio nchi adui yake mkubwa katika eneo hili.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi anamlaumu mwenziye wa Rwanda Paul Kagame kwa kufadhili jaribio la kutaka kumpindua madarakani miaka mitatu iliyopita pamoja na kutoa mafunzo kwa vikundi vya waasi vinavyovuruga usalama wa nchi hiyo.

Rwanda nayo haiko sawa na jirani zake Uganda. Mamlaka mjini Kigali zimekuwa zikilalamikia matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu dhidi ya raia wake wanaoenda Uganda.

Rwanda imekuwa ikikanusha madai ya Burundi, wakati Uganda haisemi lolote.

Ratiba ya mkutano wa leo inaonesha kuwa kutazungumziwa masuala kuhusu kuanzishwa kwa sarafu ya pamoja na masuala mengine ya kisiasa ndani ya jumuia.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *