Virusi vya Corona: Aina mbali mbali za chanjo zinazotolewa Kenya zawagawanya walio navyo na walala hoi


Serikali ya Kenya imeidhinisha matumizi ya chanjo ya Oxford-AstraZeneca

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Sputnik V inadaiwa kuwa na uwezo wa kinga wa asilimia 91.6 ilhali AstraZeneca ina kiwango cha kinga cha asilimia 76 .

Utoaji wa chanjo ya Urusi ya Sputnik V umezua mjadala mkubwa nchini Kenya kuhusu utaratibu wa kuiidhinisha na wanaopewa chanjo hiyo kwani imefungua wazi tofauti kati ya walio navyo na wasio navyo.

Inadaiwa chanjo hiyo inagharimu kati ya shilingi 6000 hadi 9000 na watu wengi walio mashuhuri ama wenye uwezo wamethibitisha kuipokea .

Hali ni tofauti na chanjo ya AstraZeneca ambayo inapewa wananchi .

Mawakili wawili mashuhuri nchini humo wamesema wazi kwamba walipokea chanjo hiyo ya Sputnik licha ya Kaimu mkurugenzi wa Afya Patrick Amoth kuwaarifu maseneta na wabunge kwamba chanjo hiyo ingali imehifadhiwa .Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *