Virusi vya corona: Idadi ya maambukizi yapanda zaidi kwa siku Uganda, huku mtu wa kwanza akifariki Rwanda


Dereva

Haki miliki ya picha
Getty Images

Idadi ya maambukizi ya Virusi vya corona imeongezeka kwa kiwango cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa siku moja nchini zaidi kwa siku Uganda, huku mtu wa kwanza akifariki Rwanda.

Miongoni mwa walioambukizwa nchini Uganda ni madereva 52 wa malori. Kati ya hao 50 waliingia nchini humo kutoka Sudan Kusini kupitia mpaka wa Elegu, na wengine wawili kutoka Kenya kupitia mpaka wa Busia.

Wengine 32 ni wale waliowahi kutangamana na watu waliothibitishwa kuwa na maambukizi.

“Wote walikuwa karantini walipofanyiwa vipimo,” ilisema taarifa iliyochapishwa katika mitandao ya kijamii ya Wizara ya Afya.

Huku hayo yakijiri, madereva wengine 51 wa malori kutoka mataifa ya kigeni waliopatikana kuwa na maambukizi ya corona walipofanyiwa uchunguzi katika vituo vya mpakani wamezuiliwa kuingia uganda na kurejeshwa katika nchi zao.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Madereva wa malori yanayofanya safari ndefu miongoni mwa mataifa ya Afrika Mashariki wamekua wakihusishwa na ongezeko la hivi karibuni la maambukizi ya Covid-19

Kifo cha kwanza kimeripotiwa Rwanda.

Wakati huo huo Rwanda imeripoti kifo cha kwanza cha virusi vya corona. Kwa mujibu wa wizara ya Afya nchini humo mgonjwa huyo alikuwa ni raia wa Rwanda mwenye umri wa miaka 65 aliyekua akifanya kazi ya udereva katika nchi jirani ambaye alirejea Rwanda baada ya kuugua sana.

”Alipokea matibabu katika kituo maalum cha matibabu ya ugonjwa Covid-19, lakini kwa bahati mbaya alifariki dunia kutokana na matatizo makubwa ya mfumo wa kupumua.” imesema taarifa ya Wizara ya Afya ya Rwanda.

Rwanda ina jumla ya wagonjwa 359 baada ya kuwapima watu 66,976. Wagonjwa 250 wamepona huku mmoja akifariki dunia.

Haki miliki ya picha
Ministry of Health Rwanda/Twitter

Image caption

Chati inayoonyesha maendeleo ya visa vya maambukizi ya virusi vya corona kwa mujibu wa Wizara ya Afya nchini Rwanda

Hivi karibuni Uganda na Rwanda zimekuwa zikihusisha maambukizi mapya ya virusi vya corona na madereva wa magari ya mizigo wanaofanya kazi baina ya mataifa ya Afrika Mashariki.

Hatua za kudhibiti corona miongoni mwa madereva

Mnamo Aprili 29, 2020, Rais wa Uganda Yoweri Museveni alitangaza hatua mpya za kudhibiti mienendo ya madereva wa malori wanaoingia nchini humo kutoka mataifa jirani baada kuthibitika wanachangia ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19.

Hatua hizo ni pamoja na kila lori kuwa na mtu mmoja – dereva pekee yake ambaye hataruhusiwa kulala hotelini wala nyumbani kwa watu.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mwezi Aprili Rais Yoweri Museveni alitangaza hatua mpya za kudhibiti mienendo ya madereva wa malori baada ya kuthibitika kuwa wanachangia maambukizi ya corona

Mataifa ya Uganda na Kenya yamekuwa yakiwafanyia vipimo wa virusi vya corona madereva wa malori katika mipaka yao.

Hata hivyo madereva na wasaidizi wao upande wa Kenya wamekuwa wakilalamikia utaratibu wa kufanyiwa vipimo vya Covid-19 ambao unachukuwa siku kadhaa kabla ya kuruhusiwa kuvuka mpaka wa kuingia Uganda.

Njia ya usafirishaji mizigo kutoka bandari ya Mombasa nchini Kenya ni muhimu sana katika usafirishaji wa bidhaa muhimu kama vile chakula na dawa hadi Uganda, Rwanda, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo.

Lakini wasafirishaji wa mizigo hiyo sasa wanahofiwa huenda wakaeneza virusi vya corona katika kanda ya Afrika Mashariki.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *