Virusi vya Corona: Je, kalenda ya Kombe la Dunia 2022 Qatar kuathrika?


Artist's impression of Qatar World Cup in 2022

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Bado hajafahamika ikiwa virusi vya corona vitaathiri michuano ya kombe la dunia nchini Qatar 2022

Virusi vya corona huenda vikaathiri kalenda ya soka ya kimataifa kwa “miaka miwili au mitatu”, amesema mwanachama wa kamati ya Uefa.

Lars-Christer Olsson, rais wa ligi za Ulaya, amesema itakuwa suala la kusubiri na kuona hali itakavyokuwa ili kuweza kutathmini athari za janga la corona ikiwemo kombe la Dunia nchini Qatar 2022.

Uefa ina matumaini ya kumaliza ligi ya Mabingwa na Europa mwezi Agosti.

Uamuzi wa iwapo hilo linawezekana au la utafanywa mwezi Mei.

Pia kuna mipanga ya kupanga michuano mara tatu badala ya mara mbili katika ngazi ya kimataifa msimu wa pukutizi kucheza Euro 2020 na michuano ya ligi ya taifa.

Olsson amesema ni kheri msimu wa sasa usimalizike badala ya kuchelewa kuanza msimu ujao”.

Kufuatia kusitishwa kwa michezo ya soka na nchi mbalimbali na michuano ya Euro 2020 na Euro 2021, aliulizwa katika warsha iliyofanyika kwenye mtandao je kalenda ya soka itaathirika kwa kiasi gani.

“Nafikiri pengine miaka miwili au mitatu,” amesema.

Awali, alikuwa ameiambia BBC Radio 5 katika kipindi cha asubuhi kwamba hakuna maridhiano kati ya nchi kwa michuano ya ndani ya nchi, kwasababu kila nchi inakabiliwa na hali tofauti kwa misingi ya ugonjwa wa corona na hatua za serikali.

Ligi mbili za juu Ufaansa Ligue 1 na Ligue 2, hazitarejelelewa msimu huu baada ya Ufaransa kupiga marufuku michezo yote ikiwemo ile inayochezwa bila mashabiki hadi Septemba.

Ligi ya Uholanzi ilisitishwa wiki jana huku kukiwa hakuna aliyepandishwa daraja wala kushushwa ama kutangazwa mshindi.

Alipoulizwa endapo wana hitimisho la kutosha kwa mashindano yao kuendelea ikiwa baadhi ya klabu zinazoshiriki kama PSG na Ajax, hazitakuwa zimecheza kwa miezi mingi amesema: “Ni jambo gumu kulizungumzia lakini katika hali yeyote ile, hili ni jambo lisilo la kawaida ambalo utatuzi wake nao utakuwa si wa kawaida.”

Akizungumza katika mkutano wa njia ya mtandao amesema: “Kwa sasa tunaendelea na mipango, tunajaribu kuminya hatua ya msimu iliobaki katika kipindi cha mwezi mmoja wa Agosti.

“Kama hilo litafanikiwa, basi nafikiri tutaweza kulinda uhalisia na sifa ya hatua ya mwisho ya msimu huu wa michuano ya kimataifa ya kandanda.

“Lakini itatupasa kuchukua hatua walau kufikia mwishoni mwa mwezi Mei kwa sababu zaidi yah apo itakuwa ngumu kuuminya msimu na kufuzu kwa klabu za msimu ujao.”

Huku michuano ya Kombe la Dunia ikiwa chini ya miaka mitatu kufanyika, Olsson aliuliza endapo pia itaathirika.

“Endapo virusi vitaendelea kusambaaa kwa kasi zaidi ya hii ya sasa, basi ni dhahiri kutakuwa na matatizo makubwa katika kalenda ya kimataifa,” amesema.

“Pale baadhi ya michuano itakapopelekwa mbele kwa mwaka mmoja zaidi kisha Kombe la Dunia Qatar linakuja katikati ya msimu wa kandanda ya Ulaya na inakupasa uminye kalenda ya michuano ya ndani nay a kimataifa hapo kutakuwa na athari. Lakini nafikiri kwanza inatupasa tusubiri na kuona ni kwa namna gani athari hizi zitaendelea.”Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *