Virusi vya corona: Je mfumo wa maisha ya shule na vyuo utabadilika vipi kutokana na virusi Tanzania?


Image caption

Wanafunzi watatakiwa kuvaa barakoa wawapo shuleni

Nchini Tanzania, maelfu wa wanafunzi wa vyuo na wale wa sekondari wanaomaliza kidato cha sita hii leo wameanza rasmi masomo yao baada ya kuwepo katika likizo ya ghafla kwa muda wa miezi miwili iliyosababishwa na kutokea kwa janga la virusi vya corona.

Serikali ya Tanzania kupitia rais wa nchi hiyo John Magufuli, ametangaza kufunguliwa kwa vyuo leo baada ya kusema kuwa amejiridhisha kwamba maambukizi ya Covid19 yamepungua nchini.

Katika baadhi ya maeneo kama vile Chuo Kikuu cha Dodoma-UDOM, wanafunzi walianza kufika chuoni hapo mwishoni mwa juma kwa ajili ya kuendelea na taratibu za usaili ili ifikapo Jumatatu, wanafunzi wawe madarasani kwa ajili ya masomo.

Mfumo wa Maisha Kubadilika

Hata hivyo, licha ya vyuo kufunguliwa, baadhi ya wanafunzi wanakiri kwamba mfumo wa maisha sasa hivi utakuwa umebadilika kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwepo kwa janga la Covid19.: “Uwepo wa ugonjwa huu utabadilisha mfumo wa maisha kwa wanafunzi. Kwa mfano uvaaji wa barakoa na kunawa mikono mara kwa mara. Lakini kuwepo kwa umbali kati ya mwanafunzi na mwanafunzi, inaweza isiwe rahisi sana kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi iliyopo,” amesema Godfrey Mwamenge, rais wa wanafunzi UDOM.

Hadija Kwezi ambae ni mwanafunzi wa Saikoloji mwaka wa kwanza, anasema tofauti na ilivyokuwa awali, hivi sasa wanafunzi wanatakiwa kuishi kwa tahadhari kwa kuhakikisha kila wakati wanavaa barakoa.

Matumaini yarejea

Kufungwa kwa shule pamoja na vyuo kumeleta athari kubwa za kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo jiji la Dodoma ambalo ni miongoni mwa mikoa yenye idadi kubwa ya vyuo nchini Tanzania. Biashara kama vile za usafiri, vyakula, na hata nguo zimeathirika kwa asilimia kubwa.

Hivyo, kufunguliwa kwa vyuo na shule, kumeanza kuleta matumaini mapya kwa jamii inayozunguka ambayo kwa kiasi kikubwa hutegemea uwepo wa wanafunzi katika biashara mbalimbali. Licha ya wanafunzi hawa kurudi vyuoni, lakini hatua kadhaa pia zimechukuliwa ili kuweka mazingira salama kwa wanafunzi ili kuepusha maambukizi ya covid19.

Image caption

Profesa Faustine Bee, Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodama amewataka wanafunzi kuzingatia uvaaji wa barakoa wanapokuwa katika maeneo ya Chuo.

Profesa Faustine Bee, Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodama amewataka wanafunzi kuzingatia uvaaji wa barakoa wanapokuwa katika maeneo ya Chuo.

“Chuo Kikuu cha Dodoma kimepokea pia maelekezo yaliyotolewa na Wizara ya Afya ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa Corona, na maelekezo haya yametolewa kwa nchi nzima, katika maagizo hayo ni pamoja na kuzingatia usafi. Katika maeneo yetu yote tutakuwa na maji tiririka, pamoja na sabuni, la pili ni kuvaa barakoa. Nitumie fursa hii kuwaomba vijana wetu wawe na barakoa zinazokubalika, zinazoweza kuwakinga, na pale maji yanapokuwa hayapatikani, wawe na vitakasa mkono. Tunaamini hakuna mwanafunzi au mtumishi atakaeugua,” amesema Profesa Bee.

Rais wa Tanzania John Magufuli amesema iwapo hali ya maambukizi itaendelea kupungua Serikali itaangalia baadae uwezekano wa kufungua shule kwa madarasa mengine. Ingawa bado serikali haijatangaza lini wanafunzi waliobaki watarudi shule, lakini baadhi ya wazazi tayari wanaonekana kuanza maandalizi kwani wanahisi wakati wowote serikali inaweza kutangaza.

Taarifa zaidi kuhusu corona:

Ni zaidi ya mwezi mmoja na wiki kadhaa sasa hivi tangu serikali ya nchi hiyo ilipoacha kutoa takwimu za kila siku zinazoonyesha maambukizi mapya.

Hata hivyo, serikali kwa mara kadhaa imesema maambukizi nchini Tanzania yamepungua kwa kiasi kikubwa hivyo kuanza kuruhusu baadhi ya shughuli kama vile usafiri wa anga, sekta ya utalii kurejea katika hali yake ya kawaida.

Hata hivyo, tofauti na ilivyokuwa awali, katika baadhi ya maeneo mwamko mwamko wa watu kuvaa barakoa umepungua, hali inayoweza kusababisha kutokea kwa wimbi jipya la maambukizi.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena

Rais wa chama cha madaktari: ‘Hospitali Tanzania hazijaelemewa na wagonjwa wa corona’Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *