Virusi vya corona : Ladha na harufu ya kuchukiza vinavyowakera baadhi ya watu waliopatwa na corona

Clare Freer, when eating out was a pleasure

Maelezo ya picha,

Clare Freer, wakati alipokua bado akifurahia chakula na mvinyo kabla ya kuugua Covid-19

Wtu wengi wenye virusi vya Covid-19 hupoteza kwa muda ladha ya vitu na harufu, wakati wanapokuwa wakipona , mara nyingi hisia hiyo hurejea- lakini baadhi wanahisi kuwa vitu vinakuwa na harufu tofauti kabisa, na vitu ambavyo vingepaswa kuwa na harufu nzuri, kama vile chakula, sabuni, na wapenzi wao, hugeuka na kuwa na harufu mbaya. Idadi ya watu wanaopatwa na hali hii inayofahamika kwa lugha ya kitaalamu kama parosmia, inaendelea kuongezeka, lakini wanasayansi wanasema hawana uhakika ni kwanini hali hii inatokea, au ni kwa jinsi gani wanaweza kuwatibu wenye tatizo hili.

Clare Freer ni mmoja wao. Amekuwa akilia kwa huzuni kila mara anapojaribu kuipigia chakula familia yake ya watu wanne.

“Harufu ya chakula hunifanya nihisi kizunguzungu . Ninapopika huwa nahisi harufu ya uozo imejaa ndani ya nyumba mara tu chakula kinapoanza kuiva kwenye jiko au kwenye oveni na hua siwezi kuvumilia ,”anasema.

Clare mwenye umri wa miaka 47-kutoka Sutton Coldfield nchini Uingereza ameishi na hali ya kuhisi chakula kinanuka kama uozo kwa miezi saba sasa na wengi waliopatwa na corona wanahisi harufu mbaya ya kunuka kila siku.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *