Virusi vya corona: Marekani iko tayari kufanya kazi bega kwa bega na Tanzania kuishinda Covid-19


Unalozi wa Marekani

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umesema kuwa Marekani iko tayari kushirikiana na Tanzania kuzuia kusambaa kwa COVID-19, na kuishinda.

Katika taarifa iliyotumwa kwenye mtandao rasmi wa Ubalozi huo, Balozi wa Marekani nchini humo Dionald Wright amesema ” Ninataka kuzungumzia kuhusu Covid-19 na jinsi tunavyoweza kushirikiana kwa pamoja kuzuia kusambaa kwake na kutusaidia sisi sote kukaa salama”

Haya yanajiri baada ya Marekani kutoa tanagazo juma lililopita ikiwatahadharisha watu dhidi ya kusafiri nchini Tanzania kutokana na corona.

Maelezo ya picha,

Hivi karibuni Rais Magufuli ashiria kubadili msimamo wake kuhusu ugonjwa wa Covid- 19

Hata hivyo hivi karibuni Tanzania imeonyesha kuimarisha juhudi za kukabiliana na virusi vya corona huku rais Magufuli akisema serikali yake haijamzuia mtu yeyote kuvaa barakoa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *