Virusi vya Corona: Rwanda yaijibu Uingereza kuhusu marufuku dhidi yake


Rwanda ni moja ya nchi chache ambazo zinazingatia kupimwa kwa Covid 19

Rwanda imesema inasubiri kupata ufafanuzi kuhusu sababu ya Uingereza kuchukua hatua ya kuiwekea marufuku ya wageni wanaosafiri au kupitia nchini Rwanda kuingia Uingereza.

Hii ni baada ya Uingereza kutangaza kuweka marufuku dhidi ya wasafiri wanaotoka Rwanda, Burundi na Umoja wa falme za kiarabu kuingia nchini Uingereza wiki hii.

Katika taarifa yake iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii, serikali ya Rwanda imesema kuwa, Rwanda imeweza kushughulia vyema udhibiti wa maambukizi ya Covid -19, ikiwa ni pamoja na kupima, kufuatilia waliokutana na wenye maambukizi, kuwadhibiti wenye maambukizi, kutibu na taarifa kuhusu zake kuhusu virusi vya corona zimekuwa za wazi na kuthibitishwa na taasisi huru.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa Rwanda ni moja ya nchi chache ambazo zinazingatia kupimwa kwa Covid 19 kwa wasafiri wote wanaoondoka na wale wote wanaopitia nchini humo kuelekea nchi nyingine.

Maelezo ya picha,

Baadhi ya Robot zinzotumiwa kuwasaidia madaktari kutibu virusi vya corona nchini Rwanda

Rwanda inasema ukizingatia orodha ya nchi za kikanda ambazo zimeathiriwa na ambazo haziojaathiriwa na marufuku, taarifa chache zilizotolewa Rwanda hazina uchunguzi wa kisayansi.

Rwanda imeikumbusha Uingereza kuwa haikujiunga na marufuku zilizowekwa na mataifa mengine za wasafiri kutoka Uingereza mwaka 2020 kutokana aina mpya ya virusi vya corona vilivyogundulika katika baadhi ya maeneo ya Uingereza.

Rwanda na Burundi zinajiunga na Tanzania, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Afrika Kusini ambazo pia zimewekewa marufuku hiyo na Uingereza.

Uingereza ilisema nini?

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Uingereza ,hatua ya hiyo inalenga kudhibiti kuenea kwa aina mpya ya kirusi cha Afrika Kusini, na marufuku hiyo inaanza kufanya kazi siku ya Ijumaa saa saba kwa saa za Uingereza.

Raia wa Uingereza, Ireland na raia wenye haki ya makazi nchini Uingereza wataruhusiwa kuingia, lakini kwa sharti la kujitenga kwa siku 10 wakiwa nyumbani.

Pia safari za moja kwa moja za ndege za abiria kutoka Uingereza kwenda Umoja wa falme za kiarabu zitapigwa marufuku.

Waziri wa usafiri Grant Shapps alisema abiria wanaoruhusiwa kuingia Uingereza watahitaji uthibitisho kuwa hawana maambukizi ya virusi vya corona kabla ya kuwasili, vinginevyo watapigwa faini ya pauni 500.

Hatua zilizochukuliwa dhidi ya Uingereza:

Uwanja wa ndege wa Dubai umesema kuwa ndege za moja kwa moja zinazotarajiwa kuwasili Uingereza baada ya saa saba, saa za Uingereza zimeahirishwa na umewaambia abiria waliokuwa wakitarajia kusafiri wasiende uwanja wa ndege.

Shirika la ndege la Etihad pia limesema ndege zake za abiria wake wanaokwenda Uingereza zitaahirishwa mpaka maelekezo mengine yatakapotolewa na wanafanya mipango na wateja wao kuhusu mipango ya kusafiri.

Jumla ya nchi 33 zimewekewa marufuku hiyo na Uingereza mpaka sasa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *