Virusi vya Corona: Serikali ya Tanzania yatangaza utaratibu wa michezo kuanzia kesho, yapi mapya?


Rais wa Tanzania John Pombe Maguful aliruhusu kuendelezwa kwa michezo mbali mbali nchini Tanzania kuanzia kuanzia Kesho Jumatatu Mosi Juni.

Haki miliki ya picha
Ikulu

Image caption

Rais wa Tanzania John Pombe Maguful aliruhusu kuendelezwa kwa michezo mbali mbali nchini Tanzania kuanzia kuanzia Kesho Jumatatu Mosi Juni.

Serikali ya Tanzania imetoa wito wa kuzingatiwa kwa mwongozo wa Afya michezoni, wakati Ligi ya soka na michezo mingine itakaporuhusiwa kuendelea nchini humo kuanzia Kesho Juni Mosi.

Hii inafuatia Maelekezo ya Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kuhuhusu michezo mbali mbali kuendelea kuanzia Kesho Jumatatu baada ya kusitishwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Kuhusu mtindo wa uendeshaji wa Ligi: ”Serikali inaruhusu ligi za soka ambazo kikanuni zinatakiwa kucheza nyumbani na ugenini utaratibu huo wa nyumbani na ugenini badala ya kituo kimoja,uendelee kutumika nchini”, imesema taarifa ya Wizara husika na michezo.

Aidha kuhusu Mashabiki serikali pia imerithia ligi zote za soka na michezo mingine kurejea, na kuongeza kuwa mashabiki watakaotaka kuhuduria viwanjani waruhusiwe kwa taratibu za kawaida isipokuwa tu kwa michezo itakayotathminiwa kuwa huenda ikajaza viwanja ambapo kanuni ya kuruhusiwa mashabiki wasiozidi nusu ya uwezo wa uwanja itumike na isimamiwe ipasavyo.

Image caption

Misongamano ya kuingia na kutoka viwanjani inatarajiwa kudhibitiwa kulingana na utaratibu mpya wa michezo nchini Tanzania

Zaidi ya hayo, mashabiki wenyewe, viongozi wa vilabu, vyama husika, watendaji wa serikali katika maeneo husika watalazimika kuhakikisha maelekezo ya Mwongozo wa Afya michezoni yanatekelezwa kikamilifu.

Miongoni mwa mwa maelekezo hayo ni pamoja na, Kuhakikisha hakuna misongamano yoyote wakati wa mashabiki kuingia na kutoka viwanjani, viwanjani watu watatakiwa kukaa na kushangilia kwa kuachana nafasi ya mita moja, kuvaa barakoa, kunawa kwa sabuni na maji yanayotiririka au vitakasamikono(sanitizer) kabla ya kuingia viwanjani na hatua kali zitachukuliwe kwa watakaokaidi hatua hizo, imesema taarifa.

Haki miliki ya picha
Ikulu

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo wadau wa michezo mingine wamekua pia wakiomba utaratibu wa kufuatwa.

Tanzania imetangaza kupungua sana kwa maambukizi ya Covid 19, jambo ambalo viongozi wa nchi hiyo wamekua wakisema ni la Kumshukuru Mungu.

Shirika la Afya Duniani pamoja na Taasisi ya udhibiti wa Magonjwa ya Muungano wa Afrika wamekuwa wakiikosoa Tanzania kwa kutotoa data za mara kwa mara za maendeleo ya Covid 19 nchini humo

Hata hivyo inakiri kuwa bado ugonjwa huo haujakwisha kabisa nchini humo sawa na nchi nyingine na hivyo wizara husika na michezo imewataka wanamichezo kila mmoja na kila kiongozi wa michezo watapaswa kujilinda na kuwakinga wengine.

Tanzania ni nchi pekee miongoni mwa mataifa ya Afrika Mashariki ambayo inafungua shughuli za michezo wakati huuambapo dunia inakabiliana na janga la corona.

Hata hivyo Ligi ya Ujerumani Bundasliga ilifungua tena michezo yake huku Ligi kuu ya Uingereza Primia Ligi ikitarajiwa pia kufungua michuano ya kuendeleza msimu.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *