Virusi vya corona: Uingereza imeruhusu matumizi ya dawa ya kukabiliana na virusi ya remdesivir


Vials of remdesivir

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Wataalamu wanaonya kuwa dawa ya remdesivir isichukuliwe kwamba ifanya miujiza ya siku moja

Tiba ambayo inaonekana kupunguza muda wa kupona unapopata virusi vya corona imeanza kupatikana katika hospitali za Uingereza.

Dawa ya Remdesivir ina kabiliana na virusi ambayo awali ilikuwa imetengenezwa kutibu viusi vya Ebola.

Wadhibiti nchini Uingereza wanasema kwamba kuna ushahidi wa kutosha wa kuidhinisha matumizi ya dawa hiyo kwa wagonjwa walio hospitali.

Kwa sababu ya muda na hali ilivyo, itawaendea wale wenye uhitaji zaidi.

Marekani na Japani pia nazo tayari zimeshafanya maandalizi ya kupata dawa hiyo mapema kabla ya kufikiwa kwa makubaliano ya kibiashara juu ya dawa hiyo.

Kwa sasa dawa hiyo inafanyiwa majaribio kote duniani ikiwemo Uingereza.

Takwimu za awali zinaonesha kwamba dawa hiyo ina uwezo wa kupunguza siku za kupona hadi nne.

Bado haijafahamika kampuni ya dawa ya Gilead Sciences ina dawa hizo kiasi gani kwa ajili ya wagonjwa wa Uingereza.

Namna ya matumizi yake itategemea kulingana na ushauri wa daktari.

Waziri anayesimamia maswala ya uvumbuzi Lord Bethell amesema: “Dawa hii inaonesha matokeo mazuri. Tunapoangazia kipindi hiki ambacho kimekuwa cha kipekee, tunatakiwa kuwa mstari wa mbele kwa maendeleo ya tiba, na kuhakikisha usalama wa wagonjwa unasalia kuwa kipaumbele.

“Yaliyotokea hivi karibuni, ushauri wa wataalamu wa kisayansi unazingatiwa katika maamuzi yote yanayofanyika na tutaendelea kufuatiliana mafanikio ya dawa ya remdesivir katika majaribio yanayofanywa kote duniani kuhakikisha matokeo bora kwa wagonjwa wa Uingereza.”

Dkt. Stephen Griffin kutoka chuo kikuu cha Leeds Medical School, amesema kuwa hii ndo dawa ambayo hadi kufikia sasa imeonesha matumaini zaidi katika magonjwa ya kuambukiza ya virusi.

Alisema wagonjwa waliougua sana ndio watakaoewa kipaumbele. “Ikiwa hii ndio dawa pekee ambayo inaonesha kuwa na matokeo mazuri, hai maanishi kwamba watu watarajie miujiza ya siku moja.

“Badala yake tunaweza kuwa na matuamini ya wagonjwa wengi kupona na kupungua kwa vifo vya watoto, tukiwa na matumaini kwamba itakuwa na manufaa kwa wagonjwa wengi zaidi.”

Dawa zingine ambazo zinafanyiwa utafiti juu ya uwezo wa kutibu virusi vya corona ni pamoja na dawa za kutibu malaria na zile za kupunguza makali ya HIV.

Dawa ya kutibu malaria ya hydroxychloroquine imesitishwa kwa baadhi ya majaribio kwasababu ya kutiliwa shaka usalama wake.

Shirika la Afya Duniani, limesema kwamba kuahirishwa kwa muda ni tahadhari, baada ya utafiti wa hivi karibuni kubaini kwamba dawa hiyo huenda inaongeza hatari ya vifo na matatizo ya moyo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *