Virusi vya Corona: Wagonjwa 12 wapya wathibitishwa Kenya


Haki miliki ya picha
Ministry of Health

Image caption

Katibu katika wizara ya afya Kenya Dkt. Rashid Aman

Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona nchini kenya, imefikia 396 amesema katibu katika wizara ya afya Dr. Rashid Aman.

Wizara ya afya imesema kwamba kati ya walipimwa, 12 wamethibitishwa kuambukizwa corona na kufikisha idadi hiyo kuwa 396.

Walioambukizwa, 7 wanatoka Mombasa, 3 Mombasa, Kitui 1 na Wajir 1.

Kwa saa 24 zilizopita, wagonjwa 15 wamepona ikiwa ndio idadi ya juu tangu kutangazwa kwa virusi hivi nchini mno huku wale waliopona ikifikia 144 kwa ujumla.

Upande wa jinsia 9 ni wanaume huku 3 wakiwa wanawake.

Aidha wawili wamethibitishwa kufa na kufikisha idadi hiyo kuwa 17.

Pia wizara ya afya imeweka wazi kwamba migahawa inayotaka kufungua tena, lazima itimize vigezo na kupata cheki kutoka kwa wizara.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *