Virusi vya Corona:Uganda imesitisha safari za ndege kutoka India baada ya kirusi cha Corona cha India kuripotiwa nchini humo


Waziri wa Afya nchini humo Ruth Aceng amesema serikali imechukua hatua mbali mbali ili kuzuia kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya virusi hivyo .

Chanzo cha picha, MINISTRY OF HEALTH UGANDA

Uganda imepiga marufuku safari zote za ndege kutoka India kuanzia saa sita usiku tarehe 1 mwezi Mei ili kuzuia wimbi jingine la janga la corona nchini humo .

Waziri wa Afya nchini humo Ruth Aceng amesema serikali imechukua hatua mbali mbali ili kuzuia kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya virusi hivyo .

Hakuna abiria kutoka India atakayeruhusiwa kuingia nchini humo bila kujali alikotokea na abiria wote waliopitia au kutoka India katika siku 14 zilziopita pia hawatakubaliwa kuingia nchini humo .

Wasafiri wote kutoka India wataaowasili Uganfda kabla ya kuanza kutekelezwa kwa marufuku hiyo watatakiwa kuwa na cheti cha kuthibitisha kwamba wamepimwa na kupatikana bila virusi vya Corona katika kipindi cha saa 120 wakati sampuli zilipochukuliwa kutoka kwao .Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *