Vita vya Yemen: Ni kwanini waasi wa Houthi wawaachilia maelfu ya wafungwa


Detainees are treated in hospital after being injured in a Saudi-led coalition air strike on a Houthi-run prison in Dhamar, Yemen (2 September 2019)

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Miongoni mwa mahabusu walioachiliwa Jumatatu ni pamoja na manusura 42 wa shambulio dhidi ya gereza la Wahouthi

Waasi wa Kihouthi nchini Yemen wamewaachilia mahabusu 290 kama sehemu ya mpango wa Umoja wa mataifa wa wa amani, kwa muibu wa shirika la Kimataifa la msalaba mwekundu (ICRC)

Wale walioachiliwa ni manusura wa 42 wa shambulio la anga dhidi ya gereza mwezi huu lililowauwa watu zaidi ya 100.

Shambulio hilo lilitekelezwa na Muungano wa Saudia unaoungwa mkono na serikali ya Yemeni katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Yemen alisema kuwa anatumai hatua ya Wahouthi itawezesha kuachiliwa zaidi kwa mahabusu wa pande zote husika na mzozo huo.

Unaweza pia kusoma:

Kubadilishana wafungwa ilikuwa ni moja ya vipengele vya makubaliano baina ya pande zinazohasimiana ambayo yaliffikiwa na Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa Sweden Stockholm, mwezi Disemba.

Mkuu wa kamati ya Wahouthi inayoshughulikia msasuala ya wafungwa wa vita, Abdul Qader al-Murtada, amesema kuwa waasi watawaachilia huru mahabusu 350 wakiwemo raia watatu wa Saudia ambao hawakutajwa majina.

“Kujitolea kwetu kunaonyesha uaminifu wetu katika utekelewaji wa makubaliano ya Sweden na tunazitolea wito pande nyingine husika kuchukua hatua kama yetu ,”aliongeza.

Baadae shirika la msalaba mwekundu la kimataifa lilitangaza kuwa lilisaidia katika kuachiliwa huru kwa mahabusu 290.

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

The Houthis urged their opponents to take a comparable step

Wahudumu wa mahabusu wamethibitisha kama mahabusu ‘ walitaka moja kwa moja kuondoka kutoka katika mji mkuu wa Sanaa unaodhibitiwa hadi nyumbani kwa au kama wangependa wahamishiwe katika eneo linalodhibitiwa na serikali.

“Kuachiliwa kwao ni hatua nzuri ambayo huenda ikachochea kuachiliwa huru kwa wengine, kuwahamisha na kuwarejesha makwao mahabusu wanaohusishwa na mzozo kulingana makubaliano ya Stockholm ,” limesema Shirika la ICRC.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa amezitolea wito pande zote husika kuhakikisha mahabusu wote walioachiliwa wanafika nyumbani salama

” Nimezikaribisha pande husika kukutana zitakapopata fursa hivi karibuni na kufufua mazungumzo kuhusu hali ya baadae katika ubadilishanaji wa wafungwa kulingana na makubaliano ya Stockholm ,” alisema.

Tangazo la Wahouthi limetolewa siku moja baada ya kutangaza kuwa wamewauwa wapiganaji zaidi ya 200 wanaounga mkono serikali na kuwakamata wengine 2,000 katika shambulio kubwa karibu na mpaka na Saudi Arabia uliopo katika jimbo la Najran.

Picha za video zilizotolewa Jumapili zilioyesha makumi ya wanajeshi waliotekwa pamoja na magari ya kijeshi.

Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

Tangazo la Wahouthi limetolewa siku moja baada ya kutangaza kuwa wamewauwa wapiganaji zaidi ya 200 wanaounga mkono serikali na kuwakamata wengine 2,000

Saudi Arabia bado haijajibu madai hayo, na hakuna duru huru zilizothibitisha hayo.

Yemeni imeharibiwa na mzozo wa kivita ambao uliongezeka zaidi mwezi Machi 2015, wakati waasi walipochukua uthibiti wa eneo kubwa la magharibi mwa nchi na kumlazimisha rais Abdrabbuh Mansour Hadi kutorokea ng’ambo.

Wakihangaishwa na kuongezeka kwa umaarufu wa kundi linaloaminiwa kuungwa mkono na kijeshi na Waislamu wa Shia nchini Iran, Saudi Arabia na maitaifa mengine manane ambayo zaidi ni mataifa ya Kisunni walianza vita vya anga vilivyolenga kuirejesha serikali ya Bwana Hadi .

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Mmoja wa mahabusu aliyeshambuliwa katika shambulio Muungao unaoongozwa na Saudia dhidi ya gereza la Wahouthi nchini Yemen (tarehe 2 Septemba 2019)

Umoja wa Mataifa unasema mapigano nchini Yemen yamewauwa raia 7,000 . Lakini waangalizi wanaamini idadi ya vifo ni kubwa zaidi. Shirika la Marekani linalochunguza maeneo ya mizozo ya silaha Armed Conflict Location and Event Data Project (ACLED) linakadiria kuwa zaidi ya raia 90,000 cna wapiganaji waliuawa katika mzozo huo wa Yemen.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe pia vimesababisha mzozo mkasa mkubwa wa kibinadamu duniani, huku maelfu ya raia wakifa kwa sababu ambazo zingeweza kuepukika with thousands of civilians dying from preventable causes, including malnutrition, , ukiwemo utapiamlo , magonjwa na afya duni.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *