Wananchi wa Zanzibar wafurahia kuachiwa viongozi wa UamshoMasheikh Farid Hadi Ahmed na Msellem Ali Msellem walirudishwa Zanzibar Jumanne, magharibi baada ya kuachiwa huru mjini Dar Es Salaam, kufuatia uwamuzi wa mkurugenzi wa mashtaka wa Tanzania Sylvester Mwakitalu kuwafutia mashtaka dhidi yao.

Wanachama wengine watano wamewasili Zanzibar Jumatano mchana ikiaminika kwamba wanaachiwa kwa makundi kama alivyosema kiongozi wao Sheikh Farid Ahmed aliyeachiwa Jumanne.

Akizungumza na Sauti ya Amerika, moja wapo ya wakili wa Masheikh hao, Abdallah Juma anasema wamefurahi kuwaona nyumbani lakini wanadhani wao mawakili wangelishirikishwa kwenye utaratibu wote wa kuachiwa huru wateja wao baada ya kuwawakilisha kwa zaidi ya miaka 9.

Masheikh hao pamoja na wafuasi wao wapatao 50 walikua wanashikiliwa gerezani kwa makosa ya ugaidi na walifunguliwa mashtaka mwaka 2014. Miongoni mwa mashtaka hayo ni pamoja na kuwaingiza watu kutoka nje kushiriki kwenye vitendo vya ugaidi. Tuhuma ambazo wote wanakanusha.

Wachambuzi wa mambo Zanzibar wanasema kuachiwa kwa viongozi hao wa kislamu huwenda inafuatia mazungumzo aliyokua nayo rais Hussein Mwinyi na viongozi wa kidini juuu ya hatima ya wanachama wa Jumiki.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *