Wanaume wapenzi wa jinsia moja walichapwa na umeme ili ''kutibu hali zao'' chuoni


” Baadhi ya nyaya za umeme kwa mara ya kwanza zilifungwa kwenye miguu yangu.

” walikuwa wakinipiga na umeme na kuendelea kufanya hivyo kwa kila baada ya sekunde 15 au 30 .”

John,ambaye sio jina lake halisi , alipitia mateso ya kupigwa na umeme katika Chuo Kikuu cha Queen University Belfast (QUB) alipokuwa mwanafunzi katika miaka ya 1960. Alionyeshwa picha za utupu za wanaume na kupigwa na umeme iwapo angeonyesha kuwa na msisimuko wa ngono.

Msemaji wa Chuo Kikuu cha QUB ameelezea kusikitishwa kwake na matumizi ya umeme kama njia ya kutibu hisia za mapenzi ya jinsia moja.

John alikuwa amekulia katika maeneo ya vijijini katika miaka 1950 katika Ireland kaskazini.

” Kanisa langu lilikuwa ni la Kiprotestant -Presbyterian, kwa hiyo ilikuwa ni jambo gumu sana kwangu nilipotambua kuwa nina hisia za kimapenzi kwa wanaume wenzangu ,” aliiambia BBC kitengo cha Ireland kaskazini.

Haki miliki ya picha
Dr Tommy Dickinson

Image caption

Dkt Tommy Dickinson anasema kuwa matumizi ya umeme kama njia ya matibabu yalizuiwa katika miaka ya 1970 nchini Uingereza

“Nilipokuwa na umri wa miaka karibu 15, niligundua kuwa mimi ni mmoja wa watu hawa wenye hisia za mapenzi ya jinsia mojana ambao wanachukiwa sana na jamii ninamokulia, lilikuwa ni pigo kubwa sana kwangu.

“Nilijihisi niko peke yangu kabisa .”

Awali John aliongea na Dkt wake ambaye alimuonea huruma na kumuandalia matibabu ya kupewa ushauru nasaha katika hospitali moja ya eneo lao.

Hata hivyo, alipojiunga na chuo kikuu katika miaka 1960 alipelekwa kwenye idara ya weney magonjwa ya akili katika chuo kikuu.

“Nilifurahi kukukubali chochote ambacho wangeniambia, nilichokitaka tu ni kutibiwa ,” alisema.

Lengo la kumpiga umeme lilikuwa ni kumfanya afananishe mapenzi ya jinsia moja na maumivu au hali isiyofurahisha.

“Nilionyesha msururu wa kitu ambacho , kwa sasa unaweza kufananisha na picha za ponografia za kiwango kidogo.

“Nilipewa viatu ambavyo vilikuwa vimechomekwa kwenye nyaya za umeme , na nilikuwa ninapigwa na umeme miguuni kupitia viatu hivyo.

“Lakishangaza ni kwamba nilikuwa ninahisi maumivu makali miguu ni mwangu, na ndipo nikafanikiwa kuwashawishi wanipige umeme kwenye mikondo yangu badala ya miguu.

” Kwa hiyo baadae walifunga kitu fulani kwenye mikono yangu ambacho kilikuwa kinasukuma nguvu za umeme ulioendelea kunipiga .”

Lilikuwa ni jambo la kutisha na baya sana

John alilazimishwa kubonyeza kikidude cha umeme kila alipohisi pale alipohisi kuwa na hisia za ngono kwa picha ya mwanaume .

” Nilipobonyeza kidudue hicho ilimaanisha kuwa nimepata hisia za ngono kw amwaname mwenzangu ,halafu baada sekunde 15 au 30 iwapo sijabonyeza wananiongezea kipigo cha umeme ,” alisema .

“Waliendelea kunipiga umeme hadi nitakapo bonyeza kidude tena kama ishara ya kusema siskii hisia tena kwa mwanaume mwenzangu.

“Ndio nilikuwa naskia maumivu makali, lilikuwa ni jambo la kutisha sana.

“Hii inakufanya ufananishe mshiriki yeyote wa mapenzi ya jinsia moja , au hisia zake na hali mbaya isiyofurahisha- hali ambayo niliihisi kusema kweli “

John pia alishawishiwa kumtafuta mpenzi wa kike wakati alipokuwa akipitia matibabu.

Katika utafiti uliochapishwa katika jarida la kitabibu mwaka la Ulster Medical mwaka 1973, wasomi kutoka idara za magonjwa ya akili , masuala ya kijamii na saikolojia katika chuo kikuu cha QUB walisema kuwa matumizi ya kupigwa na umeme kama tiba yalikuwa ni nadra kwa kiwango kama hicho.

Lakini waliendelea kutumia tu njia hiyo.

Haki miliki ya picha
PAcemaker

Image caption

Maelfu ya wapenzi wa jinsia moja wakishiriki maandamano ya wapenzi wa Belfas mwaka 2019

Msemaji wa Chuo Kikuu cha Queen cha Belfast alisema kuwa wanasikitishwa sana na matumizi ya umeme kama njia ya kutibu hisia za mapenzi ya jinsia moja.

“Hakuna ushahidi wa kisayansi wa matumizi ya tiba ya aina hiyo kwa ajili ya kubadili tabia ya mtu ,” alisema.

“Matumizi ya mbinu hizi hayajawahi kuungwa mkono na chuo kikuu cha Queen au NHS.

“Japokuwa hatuwezi kubadili tabia za vipindi vilivyopita chuo kikuu cha Queen kimejitolea kubuni na kuimarisha mazingira ya kudumu ambayo yananathamini watu wa tabaka mbali mbali .”

Tiba hiyo haikufanya kazi

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

John alipelekwa kwenye idara ya afya ya akili ya chuo kikuu cha Queen miaka ya 1960

“Hatimae baada ya miaka ya kujaribu kila niwezavyo kupokea tiba hii kwa kweli haifanyi kazi , hisia zangu kwa wanaume wenzangu ziliendelea kuwa kama zilivyokuwa mwanzo na sikuwa nawatamani wasichana kimapenzi kabisa ,” alisema.

“Ninadhani ni ujinga , ninaweza kusema nini kweli ; Ningefanya chochote kuwa mtu wa kawaida kama nilivyoono.

“Sidhani niliharibiwa na kupigwa umeme ,Sijapata mfadhaiko wa kiakili kutokana na kupigwa umeme- nimeweza kupona.

“Kwa bahati muda mfupi baada ya tiba hiyo nilikutana na wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na maisha yangu yakabadilika kabisa na tangu wakati huo mambo yamekuwa mazuri zaidi”

“Sijui watu watasema nini juu ya haya .Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *