Wazijua bidhaa tatu zilizopanda bei Tanzania, Kenya na Uganda?


  • Peter Mwangangi
  • BBC Biashara

c

Gharama ya maisha imekuwa ikiongezeka katika miezi ya hivi karibuni katika mataifa ya eneo la Afrika Mashariki ya Kenya, Tanzania na Uganda. Hizi ni baadhi ya bidhaa ambazo zimeonekana kuongezeka bei katika nchi hizo tatu:

Mafuta ya Petroli

Ongezeko hili limetokana na ongezeko la bei ya mafuta ghafi (crude oil) duniani katika miezi ya hivi karibuni, huku ulimwengu ukishuhudia ongezeko la shughuli za kiuchumi baada ya nchi nyingi kufungua biashara na kuonekana kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa corona kupitia chanjo na kanuni nyinginezo. Hali hii imepelekea hitaji la mafuta (demand) kuongezeka ikilinganishwa na uwepo wa mafuta yenyewe sokoni (supply).

Serikali za Tanzania na Kenya zimeweka mikakati ya kulinda umma dhidi ya bei za juu za mafuta, kupitia hatua kama vile kupunguza au kuondoa baadhi ya tozo na kodi kwa mafuta. Hata hivyo, bei ya mafuta bado iko juu ikilinganishwa na ilivyokuwa miezi michache iliyopita. Tuangalie hali ilivyo katika nchi zenyewe:

Chanzo cha picha, Getty Images

Tanzania: Mwezi Novemba, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilitangaza bei mpya za petroli kuwa TZS 2,439 ($1.06) kwa lita, na TZS 2,243 ($0.97) kwa lita ya dizeli mjini Dar es Salaam. Mnamo Septemba, bei ya lita moja ya petroli ilikuwa Tsh 2511 ($1.09), huku dizeli ikiuzwa 2291 ($1.00) kwa lita mjini Dar Es Salaam.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *