Waziri Mkuu wa Iraq kujiuzulu baada ya watu kupoteza maisha wakati wa maandamano


Bwana Abdul Mahdi

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Seriklali ya Abdul Mahdi imekosolewa na kiongozi mkubwa wa kidini wa kishia nchini Iraq

Waziri Mkuu wa Iraqi Adel Abdul Mahdi anatarajiwa kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu, ofisi yake imeeleza, baada ya zaidi ya watu 40 kuuawa ndani ya siku moja tangu kuanza kwa maandamano ya kuikosoa serikali.

Kiongozi wa juu wa kiislamu wa madhehebu ya Shia amekemea matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji na kutaka kuwepo kwa serikali mpya.

Karibu watu 400 wameuawa wakati wa maandamano tangu mwanzoni mwa Oktoba, na takribani watu 15 waliuawa siku ya Ijumaa.

Raia wa Iraq wanataka kazi na kukomesha vitendo vya rushwa pia huduma nzuri kwa Umma.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema ”amesikitishwa sana na ripoti kuhusu muendelezo wa matumizi ya silaha dhidi ya waandamanaji” na kutaka matukio hayo yakome.

Kwanini Abdul Mahdi anajiuzulu?

Taarifa yake inasema atawasilisha waraka wake wa kujiuzulu bungeni ili wabunge wachague serikali mpya.

Uamuzi huo umekuja baada ya Kiongozi wa juu wa kidini Ayatollah Ali al-Sistani kutaka kuanzishwa kwa serikali mpya.

”Nikichukua hatua baada ya wito huu, na ili kuhakikisha linafanyika kwa haraka, nitawasilisha bungeni waraka wa kukubali kujiuzulu nafasi yangu ya uongozi wa serikali ya sasa,” taarifa yake iliyotiwa saini na bwana Abdul Mahdi ilieleza.

Taarifa haikusema atajiuzulu lini. Jumapili bunge litakaa kwa dharura kujadili hali ilivyo nchini Iraq.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Mazishi ya mwanandamanaji mjini Najaf

Mapema siku ya Ijumaa Ayatollah Sistani alisema serikali inaonekana ”imeshindwa kushughulikia matukio yaliyojitokeza kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita”.

Kiongozi huyo amesema mashambulizi dhidi ya waandamanaji ”ni marufuku” na pia amewataka waandamanaji kuepuka vurugu na ”kuacha vitendo vya uhalifu”.

Huwezi kusikiliza tena

Bajaj zimekuwa mkombozi kwenye maandamano nchini Iraq

Bwana Abdul Mahdi alishakuwa na nia ya kujiuzulu kabla lakini kuingilia kati kwa kiongozi wa kidini, kunafanya mambo kuwa tofauti hivi sasa.

Kinachotokea Iraq ni sehemu ya wimbi la maandamano katika eneo la ukanda, miongoni mwa maandamano hayo yanasababishwa na hasira ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 30 ambao wamechoshwa na hali ya ukosefu wa ajira, huduma mbovu za umma na vitendo ya rushwa vinavyodaiwa kufanywa na viongozi nchini humo.

Kuhusu Abdul Mahdi

Abdul Mahdi alishika nafasi hiyo kipindi cha mwaka mmoja uliopita, akiahidi mabadiliko ahadi ambayo haijatekelezwa. Vijana wa Iraq waliingia kwenye mitaa ya Baghdad kwa mara ya kwanza mwanzoni mwa mwezi Oktoba.

Baada ya maandamano ya kwanza yaliyodumu kwa siku sita na kugharimu maisha ya watu 149 Mahdi aliahidi kufanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri na kupunguza mishahara ya maafisa wa juu, na alitangaza pia kushughulikia suala la ukosefu wa ajira.

Lakini waandamanaji wanasema kuwa matakwa yao hayajatimizwa na kurejea tena mitaani mwishoni mwa mwezi Oktoba. Maandamano yalifanyika nchi nzima baada ya maafisa wa usalama kutumia nguvu kuwadhibiti waandamanaji.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Maandamano zaidi yalifanyika mjini Najaf siku ya Ijumaa

Kilichotokea siku ya Alhamisi

Mkurugenzi wa utafiti kutoka Amnesty International eneo la Mashariki ya kati, Lynn Maalouf, amevishutumu vikosi vya usalama kutumia nguvu siku ya Alhamisi dhidi ya waandamanaji:

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Maandamano mjini Nasiriya

  • Karibu watu 25 waliuawa mjini Nasiriya baada ya vikosi vya usalama kuwafyatulia risasi waandamanaji. Waandamanaji walilipa kisasi kwa kukichoma kituo cha polisi.
  • Waandamanaji 10 walikufa katika mji wa Najaf baada ya polisi kutumia nguvu kufuatia kuchomwa kwa ofisi ya ubalozi ya wa Iran.
  • Waandamanaji wengine wanne walipoteza maisha mjini Baghdad wakati waandamanaji walipojaribu kuvuka daraja kuelekea eneo liitwalo ‘green zone’ ambalo mikutano ya bunge hufanyika.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *