Yajue maeneo ambayo ni marufuku kufunika uso


A woman wearing a niqab looks on during a protest by a French-Algerian businessman and political activist, on October 3, 2018 in St. Gallen by following a massive vote in the Swiss northeastern canton of St. Gallen to prohibit all face-covering garments in public spaces.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Marufuku ya mavazi yanayofunika uso hadharani imekuja mara baada ya mashambulio ya kujitoa muhanga kutokea Sri lanka katika sikukuu ya Pasaka yaliosababisha vifo vya watu 250 na mamia wengine kujeruhiwa.

Vazi lolote ambalo linamficha mtu asijulikane ni nani, limekatazwa kwa mujibu wa sheria ya dharura iliyopitishwa ili kuhakikisha usalama wa taifa, kwa mujibu wa ofisi ya rais.

Wale ambao wanaunga mkono katazo hilo wanasema ni muhimu hatua hiyo kuchukuliwa kwa manufaa ya usalama wa umma na kuhamasisha maelewano yasiyo kuwa na kipingamizi kutoka kwa wachache kutokana na dini au utamaduni wa mtu .

Lakini makundi ya haki yanasema huu ni ubaguzi dhidi ya wanawake wa kiislamu, baadhi ya watu huwa wanaona mavazi haya kuwa ni wajibu wa dini zao.

Mahali gani kwingine duniani ambapo wamezuia mavazi hayo kwa kupitia sheria iliyowekwa na bunge au chini ya sheria ya dharura?

Bara la Ulaya

Ufaransa ni nchi ya kwanza Ulaya kupiga marufuku mavazi ya kiislamu yanayofunika uso wote katika maeneo ya umma mwaka 2011 kufuatia kura zilizopigwa bungeni mwaka 2010.

Marufuku hiyo ilikubaliwa na mahakama ya haki za binadamu barani ulaya mwezi July mwaka 2014.

Marufuku nyingine ya kufunika uso ilisababisha maandaano Denmark ilipoanza kufanya kazi mwezi agosti mwaka 2018.

Sheria inasema kwamba mtu yeyote anayevaa vazi linalomficha sura yake katika maeneo ya umma anapaswa kulipa faini ya dola 157 ambayo iko juu sana kama mtu atakuwa amefanya makosa ya kujirudia.

Seneta wa Netherlands alipitisha sheria hiyo mwezi Juni 2018 kwa kupiga marufuku watu wasijifunike sura zao hadharani kama katika shule na hospitalini na kwenye vyombo vya usafiri vya umma lakini sio sheria hiyo haiwahusu watu mitaa.

Ujerumani ni marufuku kwa watu kufunika nyuso zao wakiwa wanaedesha magari.

Bunge la Ujerumani limeidhinisha kuwapiga marufuku watumishi wa umma, askari na mahakimu .

Wanawake ambao wanavaa mavazi yanayowafunika nyuso zao wanapaswa kuyaacha ili waweze kutambulika.

Mavazi yot yanayofunika uso yamekatazwa katika mahakama na kulazimishwa kukatazwa shuleni nchini Austria mwezi oktoba mwaka 2017.

Ubelgiji ilianza kufanyia kazi marufuku hiyo Julai mwaka 2011.

Sheria ilipitishwa Norway mwezi Juni 2018 kwa kukataza mavazi hayo yasivaliwe katika taasisi za elimu.

Bunge laBulgaria‘lilipitisha sheria hiyo mwaka 2016 na watakaokiuka kulipa faini.

Hali ni hiyo hiyo huko Luxembourg, ambapo si ruhusa mtu kuonekana hospitalini, mahakamani na kwenye majengo yoyote ya umma mtu kuonekana amejifunika uso wake.

Baadhi ya nchi za ulaya kuna nchi ambazo zimeweka marufuku katika baadhi ya miji tu.

Hii ni pamoja na Italy, ambapo miji kadhaa imepiga marufuku watu kufunika nyuso zao na walianza kutekeleza katazo hilo mwaka 2010.

Huko Spain, katika mji wa Barcelona , marufuku ya mavazi yanayofunika uso yalianza mwaka 2010, katika baadhi ya maeneo ya umma kama sokoni na maktaba.i

Baadhi ya maeneo ya Switzerland.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Afrika

Mwaka 2015, baada ya mashambulizi kadhaa ya kujitoa mhanga yaliyofanywa na wanawake walikuwa wamevaa mavazi ya kufunika uso yalisababisha nchi kama Chad, Gabon, maeneo ya magharibi ya Cameroon, Niger‘ katika mji wa Diffa na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Algeria, iliweka katazo ya mavazi hayo mwezi Oktoba 2018.

China

Mavazi ya kufunika uso ni marufuku pamoja na kufuga ndevu nyingi.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *