Orodha mpya ya mabilionea Afrika yamshirikisha Dangote na Mo Dewji


Aliko Dangote

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Mtu tajiri zaidi barani Afrika Aliko Dangote

Mfanyibiashara Mohammed Dewji kutoka Tanzania ametajwa kuwa miongoni mwa mabilioni 20 wa Afrika katika ripoti ya jarida la Forbes la mwaka 2020.

Katika ripoti hiyo mfanyabiashara tajiri nchini Nigeria Aliko Dangote ameorodheshwa kwa mara ya tisa mfululizo, kuwa mtu tajiri barani Afrika .

Dangote mwenye umri wa miaka 62 ambaye anafanya biashara ya Simiti, Sukari na unga wa ngano ana utajiri wa dola Bilioni 10.1.

Pia unaweza kusoma:

Dangote anafuatiwa na mfanyabiashara wa Misri Nassef Sawaris ambaye aliongeza utajiri wake kutoka dola bilioni 6.3 hadi dola bilioni nane.

Mfanyabiashara huyo anamiliki asilimia 5.7 katika kmapuni ya viatu ya Adidas . Ongezeko la hisa za Adidas liliomuongezea dola bilioni moja nukta tano katika akaunti yake.

Haki miliki ya picha
HAKI MILIKI YA PICHAAFP/GETTY IMAGES

Image caption

Bilionea kutoka Tanzania Mo Dewji

Bilionea aliyeorodheshwa katika nafasi ya tatu ni raia wa Nigeria Mike Adenuga ambaye utajiri wake unatokana na sekta ya mawasiliano na mafuta. Kampuni yake ya mawasiliano ya simu Globacom ndio ya tatu kwa ukubwa nchini Nigeria ikiwa na wateja milioni 43.

Alijipatia utajiri wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 26 akiuza kanda za viatu na vinywaji.

Bilionea aliyeorodheshwa wa nne barani Afrika ni mfanya biashara wa almasi na raia wa Afrika Kusini Nicky Oppenheimer.

Nicky ambaye ni mrithi wa mali ya familia yake ya Oppenheimer ana utajiri wa dola bilioni 7.7.

Familia yake imekuwa ikihusika na uuzaji wa almasi.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *